Thursday, January 22, 2015

DUDE ASEMA ANAKUBALIANA NA STEPS KUUZA FILAMU MOJA TSH 1500

Msanii wa filamu nchini Dude amefunguka kwa kusema kuwa kwa kua serikali imeshindwa kupambana na wezi wa kazi za wasanii ni bora bei walipanga steps tsh 1500 ikubaliwe ili kuiokoa tasnia hiyo

Dude amesema hakuna njia kwa sasa ya kupambana na maharamia zaidi ya kushusha bei ya filamu

"tumeshindwa kuwathibiti pirates wanauza kazi kwa bei rahisi leo ukienda Buguruni unapata kazi kwa elfu mbili mpaka elfu moja miatano filamu ambayo inauzwa dukani sh elfu tano wenzako wanauza elfu mbili,kwakua watanzania wengi ni masikini hawana uwezo wa kununua filamu kwa elfu tano dukani hawana kwa kuwa wanaipata filamu hiyo hiyo kwa bei ya elfu moja na miatano

Hicho ndio kinachotuuma sana na kwakua serikali imeshindwa kuthibiti pirates mimi kwa uapande wangu steps kushusha bei ni sawa kwa sababau tunapambana na wezi wa kazi zetu,watanzania wanaoishi chini ya dola moja ndio wanunuzi wakazi zetu sisi kazi zetu hazinunuliwi na watu wa Masaki,watu wetu ni Wananyamala,Magomeni,Gongo la mboto watu ambao wanakipato cha chini sasa mtu kama huyo kweli atumie elfu tano yake kununua filamu?ni wachache wanafanya hivyo ndio maana wanakimbilia kunua filamu za  bei ya chini,kwa hiyo mimi steps naona wamechukua uamuzi mzuri ambao una manufaa kwetu na kwao pia

Siku chache zilizopita Dude alinukuliwa na baadhi ya Magazeti akipinga steps kushusha bei lakini baadae alisema hakuongea chochote na kuwa magazeti yaliandika bila ridhaa yake,hivyo binafsi msimamo wake kwenye bei ndio huo.





No comments:

Post a Comment