Monday, June 30, 2014

WASTARA:nitaendelea kuibua watoto wadogo wenye vipaji kama moja ya kumuenzi marehemu Sajuki

Mcheza filamu mkubwa Tanzania aneaminika na kupendwa na karibu nchi nzima kwa uwezo wake wakuigiza na tabia njema aliyonayo Wastara Juma Issa amesema anaendelea kuibua watoto wadogo wenye vipaji kama moja ya kumuenzi marehemu Sajuki aliyekuwa mume wake
Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwakua yupo nchi huru amesema kwenye filamu yake mpya Last Decision inayotoka hivi karibuni ameibua kipaji kingine ambacho anaamini kitakua gumzo siku za usoni

"nimecheza na binti mdogo anaitwa Leyla Issa Juma Issa na kweli ameonesha uwezo mkubwa wa kuigiza na hii ni moja yakumuenzi marehemu mume wangu kama utakumbuka filamu zetu nyingi tulikua tunacheza na binti mdogo Amida hivyo nimeamua kucheza na binti huyu kama njia ya kufata baadhi ya mema aliotuachia


Kwenye filamu hiyo pia wamo wakali wengine kama Hemed Suleiman na Edward Freedom kutoka Mwanza

No comments:

Post a Comment