Thursday, March 20, 2014

MSANII BEN ASAKWA KWA KUJERUHI

MSANII wa filamu za Kibongo , Abdulmalick
Ahmed ‘Ben ’ anasakwa na jeshi la polisi
akidaiwa kumjeruhi mzazi mwenziye, Leyla
Abdalah, mkazi wa Magomeni - Mikumi, Dar.


Msichana aliyejeruhiwa na msanii
Abdulmalick Ahmed ‘ Ben

Akizungumzia tukio hilo , Leyla alisema
mwigizaji huyo ambaye pia hufahamika kwa
jina la Serengo amekuwa akimfanyia fujo
mara kwa mara kwani Januari , mwaka huu ,
akiwa katika Ukumbi wa Travertine ,
Magomeni , Dar, alikutana na msanii huyo
ambaye alimlazimisha waondoke pamoja,
alipokataa akaanzisha vurugu.
Leyla alisema kwa kuwa msanii huyo
walishamwagana kwa talaka tatu miaka
mitatu iliyopita , alikataa kuondoka na mzazi
mwenziye huyo na kudai mbali na kuachana
naye, alikuwa na mpenzi wake mpya .
“ Nilimuambia siwezi kwenda naye popote,
alinivamia na kuanza kunishushia kipigo
kikali na kunichania nguo mbele za watu ,
wadau walijaribu kugombelezea sikujisikia
poa ndipo nikakimbizwa Hopitali ya
Magomeni , Dar nikalazwa wodi ya
mapumziko , nikatoka , ” alisema Leyla na
kuongeza:
“ Nikiwa katika maumivu ya kipigo hicho ,
Jumamosi iliyopita Ben alinishushia tena
kipigo cha mbwa mwizi baada ya kukutana
naye kwenye Baa ya Kilimanjaro ,
Magomeni - Mapipa




Abdulmalick Ahmed ‘ Ben ’ .
“ Anilikuta na wenzangu , akanivamia tena na
kuniambia anataka tuondoke, nilipomuuliza
twende wapi, akanijibu kwa ukali weee
twende tu, nikamkatalia , akapanda juu ya
meza na kunijeruhi kichwani na kiti ndipo
nikaona bora nikimbilie Kituo cha Polisi cha
Magomeni .
“ Nilimfungulia kesi kwenye jalada lenye
namba MG /RB/1234 /14 SHAMBULIO LA
KUDHURU MWILI , ” alisema Leyla . Gazeti hili
lilimtafuta Ben nakumsomea madai ya
mzazi mwenzake huyo ambapo alikiri kuzaa
naye na kudai migogoro hiyo inasababishwa
na yeye kudai mtoto wake .
“ Huyo mwanamke ni kweli nilizaa naye
lakini kwa sasa sina haja naye hata kiduchu,
nina mwanamke yuko bomba ile kinoma
ukimuona mwenyewe utabloo , siwezi
kurudia matapishi .
“ Huyo anataka kuniharibia tu , kila
nikimfuata anipe mtoto wangu anajifanya
mpana na kuniletea ndivyo sivyo ndiyo
maana tunakwaruzana mara kwa mara, ”
alisema Ben

No comments:

Post a Comment