Thursday, December 19, 2013

Irene Paul akerwa na mfumo wa kuwa na part 1na 2 kwenye filamu za kitanzania

Msanii nyota wa filamu za kitanzania Irene Paul ameponda staili ya filamu za kitanzania kutoka sehemu ya kwanza na ya pili na kubatizwa jina la part 1 na Part 2 amesema kuwa zimekuwa ni kikwazo kwa filamu hizo kushiriki katika matamasha na tuzo zinazoandaliwa nje ya Tanzania, anasema nashangaa kwani hakuna sehemu nyingine ya mfumo huo ispokuwa Tanzania pekee.

"Hakuna sababu ya filamu moja kukatwa na kuwa na sehemu mbili yaani Part 1 na Part 2 ukituma katika matamasha ya tuzo nje unapata usumbufu inabidi inakuchukua muda kwa marekebisho wakati ilikuwa jambo rahisi kuwa na Dvd moja tu unajaza fomu na kutuma sehemu husika" alisema Irene Paul akizungumza na mtandao wa Filamucental
 
Msanii huyo anasema kuwa hivi karibuni alikuwa anafuatilia filamu yake kuipeleka katika tamasha fulani kubwa la filamu alikutana na usumbufu ambao anaamini ni mfumo uliowekwa na wafanyabiashara wachache ambao wananufaika na mfumo huo wa kutoa Dvd sehemu mbili kwa filamu moja na kubatiza jina la part 1 na Part 2.
Irene anasema kajifunza mengi kwa wenzetu waliosonga mbele katika masuala ya filamu huku sisi Tanzania tukipigania hatua kwa taratibu kuelekea katika medani za kimataifa.

No comments:

Post a Comment