Kwenye filamu hiyo ya kampuni ya JB, Jerusalem Film Company na iliyoongozwa na Adam Kwambiana na John Kalaghe, Jokate ameigiza kwa jina la Ndekwa.
“Richie ameigiza kama rafiki yake na kaka yangu ambaye anatoka vilevile na wifi yangu na baadaye ananitaka mimi na tunaishi pamoja lakini vitu haviendi sawa,”
“Wifi yangu atakuja na atakuwa anamtishia maisha sababu yuko na mimi. So kidogo yupo kama half my boyfriend, half my protector but sio mtu ninayempenda.”
Irene Uwoya ndiye aliyeigiza kama wifi yake na Jokate kwenye filamu hiyo
Jokate amesema wakati wa kushoot filamu hiyo alikuwa akijikuta akichoka mno kwakuwa hajaagiza kwa kipindi kirefu na shughuli ilikuwa ikichukua siku nzima na nusu.
“Naweza nikaondoka home saa moja, narudi saa 10 usiku kwahiyo nilikuwa nachoka sana. Nilikuwa nafanya kazi sana, kwangu mimi kidogo ilikuwa inanisumbua. Lakini watu katika kampuni ya JB walikuwa wakiniattend vizuri, nikichoka wanasikiliza, nakula nini, maji whatever kwahiyo at least walinipa wepesi katika kucheza character yangu.”
No comments:
Post a Comment