DIVA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya urembo na mitindo Bongo, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa ‘drama’ zinazoendelea kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi nyingi hazina ukweli na ukweli anao moyoni.
Akipiga stori ‘direct’ na gazeti hili hivi karibuni, Jokate alikiri kuwa ana mpenzi ambaye anampenda sana lakini kwa bahati mbaya mpenzi huyohuyo anamuumiza sana lakini akakataa kumtaja jina alipobanwa na mwanahabari wetu.
“Kiukweli mtu niliyenaye ni sahihi kwangu, ninampenda sana japo na yeye kuna namna fulani ananitesa lakini kiukweli kwake nimefika na Mungu akipenda si muda mrefu watu watamfahamu,” alisema Jokate.
Hata hivyo, miezi ya hivi karibuni Jokate alikuwa akibanjuka kimalovee na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ ambaye inasemekana wameshamwagana.
No comments:
Post a Comment