Monday, January 06, 2014

Matapeli wa “facebook“watumia jina la Mh mbunge Halima Mdee vibaya soma statasi hii hapa chini

Kijana Ally Rajabu Mshirazy ametumiwa ujumbe “facebook“na mtu anaetumia akaunti yenye jina la Mh Mbunge Halima James Mdee na kuombwa shilingi 30000,samo post ya kijana huyo baada ya kugundua ni matapeli

Jaman wale wadau wa fb,kuna mtu anajiita HALIMA JAMES MDEE huyu ni tapeli anaetumia jina la mhe mbunge mdee humu fb,

Leo ameniinbox na kuniomba nimuazime buku30 yupo bungeni na mdogo wake ni mgonjwa na hela hana

Kwakua mm ni mtaalamu wa intelijinsia nkamwambia nipe namba yako ya tgo nkutumie(nia yangu ni kutaka kujua jina lake)

Fasta akatuma namba 0717222573 yenye jina la EDITH NKONDOLA,

Nkamwambia ww ni tapeli na nlishackia habar zako kitambo so kwakua nimepata namba na jina lako, jiandae kupambana na mkono wa dola, lazima nikushughulikie!

Alivyoona hivyo akaniblok fastaaa!!

So jamani muwe makini na haya majina ya watu maarufu,ni matapeli tu wanatumia majina ya watu!!

Hivi mhe Halima Mdee anawezaje kuniinbox mkulima km mie na kuniomba 30,000?? ...halafu haya matapeli hayajui hata techniques za kutapeli,

Nawasilisha,
Yesterday at 7:18pm

Imetoka facebook

No comments:

Post a Comment