Mchekeshaji mkongwe wa Tanzania Rashidi Mwishehe aka Kingwendu amedai kuwa sanaa ya vichekesho Tanzania haiwalipi vizuri wasanii hao.
Akiongea kupitia Hatua Tatu ya 100.5 Times Fm, Kingwendu amesema kutokana na kipato kidogo wanachokipata wasanii hao, hujikuta wakitengwa na wasanii wenzao wa Bongo Movies ambao huingiza kiasi kikubwa cha pesa kwa kucheza movies hizo.
“Kwa kweli tasnia yetu ya filamu upande wa comedy haitulipi vizuri na ndio maana wasanii wengi wa comedy hatuna magari, hatuna nyumba nzuri, tunachokipata tunakaa na watoto wetu hivyo hivyo tunakula. Lakini kiukweli kabisa filamu ya comedy haitulipi vizuri, wanatulalia sana.”
Kingwendu ameongeza kuwa wasanii wa comedy wanatengwa na waigizaji wenzao kwa kuwa wao ni masikini.
“Kwa sababu sisi wanatutenga kwa sababu kama nilivyokwambia, ni masikini. Hatuna usafiri, na usafiri wetu sanasana mtu akijitahidi kwa comedy utakuta Kingwendu ana pikipiki. Lakini wenzetu utakuta wana ma-Hammer, wanaendesha magari mazuri mazuri.
“Japo mashabiki wanasema kuwa wanauzia sura yale magari sio ya kwao, lakini sisi tunaamini ni ya kwao kwa sababu filamu wanauza kwa bei nzuri sana. Hasa kwenye soko la Steps pale wanauza kwa bei nzuri sana kama una filamu nzuri.”
Mchekeshaji huyo amewashauri wasanii wa Bongo Movie kuwa wamoja na kutowatenga wachekeshaji kwa kuwa ubaguzi huo utaipoteza tasnia ya filamu Tanzania.
Friday, December 20, 2013
“Comedy hatulioi vizuri,tunadharaulika,waigizaji wenzetu wanatutenga kwa sababu ni masikini“kingwendu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment